Kiungo wa Federico Valverde wa Real Madrid amepata jeraha la kifundo cha mguu daraja la tatu (Grade 3 ankle sprain).
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, majeraha ya aina hiyo yanaweza kumlazimu mchezaji kuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha takribani miezi 2 hadi 3, ingawa muda halisi wa kupona hutegemea maendeleo ya matibabu na hali ya jeraha.
Valverde ni miongoni mwa wachezaji muhimu wa Real Madrid, hivyo kutokuwepo kwake kwa muda huo kunaweza kuathiri kikosi katika kipindi kijacho.



