Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Dorothy Semu, amefanya mabadiliko katika Baraza Kivuli la Mawaziri la chama hicho, kwa kuteua mawaziri wapya katika wizara tatu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Alhamisi, Septemba 24, 2026, na Katibu Mkuu Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Idrisa Kweweta, mabadiliko hayo yamefanyika baada ya mashauriano kati ya Semu na Waziri Mkuu Kivuli, Ishaka Mchinjita.
Katika mabadiliko hayo yaliyoanza kutumika mara moja, Wakili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Emmanuel Lazarus Mvula, ameteuliwa kuwa Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria.
Mvula anarejea katika nafasi hiyo baada ya awali kuhudumu kama Waziri Kivuli wa Fedha na Ardhi kati ya mwaka 2022 na 2025.
Hussein H. Kalyango ameteuliwa kuwa Waziri Kivuli wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, akitokea katika nafasi ya Naibu Waziri Kivuli wa Ulinzi na Mambo ya Ndani.
Aidha, Dickson Modestus Kilufi ameteuliwa kuwa Waziri Kivuli wa Kilimo, Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi.
ACT-Wazalendo imesema uteuzi huo ni sehemu ya mabadiliko katika muundo wa Baraza Kivuli la Mawaziri linalolenga kuisimamia na kuikosoa Serikali katika utekelezaji wa majukumu yake.






