SalambaTV
NyumbaniHabariJamvikaRatibaRedio
  • Top Stories
  • Breaking News
  • Transfers
  • NBC Premier League
  • Match Highlights
  • Fixtures & Results
  • Standings & Tables
  • Tactical Analysis
NyumbaniHabariJamvikaRatibaRedio
SalambaTV
Ingia
Rudi nyumbani
Ingia

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Salamba TV· Top Stories· 16 Oktoba 2026· 2 dakika za kusoma· 188 wasomaji
SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Serikali imesisitiza kuwa itaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji wanaotekeleza miradi ya maendeleo, huku ikihakikisha sheria na taratibu za utunzaji wa mazingira zinafuatwa ili kulinda rasilimali za nchi.

Kauli hiyo imetolewa Oktoba 15, 2026, jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Reuben Kwagilwa, wakati akiwasilisha maoni ya Serikali mbele ya Kamati za Kudumu za Bunge za Maji na Mazingira pamoja na Miundombinu.

Majadiliano hayo yalihusu ombi la Chama cha BOPOA–Lake Zone la kutaka kufanyiwa mapitio kifungu cha 57(1) cha Sheria ya Usimamizi wa Mazingira na kanuni zake, ili kuruhusu matumizi maalumu ya ukanda wa mita 60 kwa shughuli za kibandari, kwa kuzingatia Tangazo la Serikali Na. 293 la mwaka 2022.

Kwagilwa alisema Serikali inaendelea kusimamia shughuli za kibandari nchini ili zifanyike kwa kuzingatia sheria zilizowekwa, huku ikihimiza ushirikiano kati ya taasisi za umma na sekta binafsi katika kukuza uwekezaji.

Alifafanua kuwa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) halipo kwa lengo la kuzuia miradi ya maendeleo, bali kuhakikisha wawekezaji na wadau wengine wanatekeleza shughuli zao kwa kuzingatia sheria na kulinda mazingira.

Aidha, alisema Serikali inatambua mchango wa bandari katika kukuza uchumi na kuongeza mapato ya taifa, hivyo itaendelea kushirikiana na sekta binafsi kuboresha miundombinu ya bandari na kuimarisha ufanisi wa shughuli za kibandari nchini.

Alisema hatua hizo zinalenga kuongeza ufanisi, kuvutia uwekezaji na kuimarisha mchango wa usafiri wa majini katika maendeleo ya taifa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Selemani Kakoso, alisema uharibifu wa mazingira unaoendelea unaonesha umuhimu wa kuwepo kwa usimamizi madhubuti ili kurejesha maeneo yaliyoathirika katika hali nzuri.

Kakoso, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tanganyika, alisema ingawa uwekezaji ni muhimu katika kukuza uchumi na kuharakisha maendeleo ya nchi, wawekezaji wanapaswa kuzingatia sheria na miongozo iliyowekwa.

Aliwataka wadau kushiriki kikamilifu katika vikao vya Bunge vinavyohusu mapitio na marekebisho ya sheria mbalimbali ili maoni yao yaweze kuzingatiwa katika kuboresha sheria hizo.

Vilevile, aliielekeza BOPOA–Lake Zone kuhakikisha shughuli zake zinafanyika kwa kuzingatia sheria na miongozo ya mazingira, pamoja na kushirikiana kwa karibu na NEMC katika usimamizi na uhifadhi wa mazingira.

Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira, Jackson Kiswaga; Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile; Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia masuala ya Mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Maduhu Kazi, pamoja na wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Wakala wa Meli Tanzania (TASAC), Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), NEMC na BOPOA–Lake Zone.

0 Hifadhi

Habari zinazohusiana

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

Top Stories · 20 Okt

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

Top Stories · 16 Okt

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

Top Stories · 16 Okt

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

Top Stories · 16 Okt

FAO YAWATAKA WALIMU NA WAZAZI KUENDELEZA VIPAJI VYA WANAFUNZI

FAO YAWATAKA WALIMU NA WAZAZI KUENDELEZA VIPAJI VYA WANAFUNZI

Top Stories · 16 Okt

© 2026 Salamba TVMasharti ya matumiziSera ya faraghaSera ya marejeshoBeti kwa kuwajibika. Watu wazima 18+ pekee.

Shiriki kwa

Habari zinazohusiana

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

Top Stories · 20 Okt

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

Top Stories · 16 Okt

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

Top Stories · 16 Okt

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

Top Stories · 16 Okt

FAO YAWATAKA WALIMU NA WAZAZI KUENDELEZA VIPAJI VYA WANAFUNZI

FAO YAWATAKA WALIMU NA WAZAZI KUENDELEZA VIPAJI VYA WANAFUNZI

Top Stories · 16 Okt

Zaidi kutoka

Top Stories →