SalambaTV
NyumbaniHabariJamvikaRatibaRedio
  • Top Stories
  • Breaking News
  • Transfers
  • NBC Premier League
  • Match Highlights
  • Fixtures & Results
  • Standings & Tables
  • Tactical Analysis
NyumbaniHabariJamvikaRatibaRedio
SalambaTV
Ingia
Rudi nyumbani
Ingia

FAO YAWATAKA WALIMU NA WAZAZI KUENDELEZA VIPAJI VYA WANAFUNZI

Salamba TV· Top Stories· 16 Oktoba 2026· 2 dakika za kusoma· 94 wasomaji
FAO YAWATAKA WALIMU NA WAZAZI KUENDELEZA VIPAJI VYA WANAFUNZI

Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) nchini Tanzania limewataka walimu na wazazi kushirikiana katika kutambua na kukuza vipaji vya wanafunzi ili kuwawezesha kutumia uwezo wao kuchangia maendeleo ya taifa.

Wito huo umetolewa Oktoba 14, 2026, na Mwakilishi Msaidizi wa FAO nchini Tanzania, Charles Tulahi, wakati wa mashindano ya uchoraji yaliyoandaliwa na shirika hilo katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara, jijini Tanga, ikiwa ni sehemu ya maonesho ya Siku ya Chakula Duniani.

Tulahi amesema mashindano hayo yanatoa nafasi kwa wanafunzi kuonesha ubunifu wao na kujifunza namna wanavyoweza kutumia vipaji vyao kuhamasisha jamii kuhusu masuala ya chakula na lishe.

Amewahimiza wanafunzi kuendeleza uwezo wao hata baada ya mashindano, ili waweze kuwa mabalozi wa ubunifu na kuifikishia jamii ujumbe kuhusu umuhimu wa upatikanaji wa chakula bora na lishe.

Ameongeza kuwa ubunifu wa wanafunzi una nafasi muhimu katika kuchangia upatikanaji wa chakula na kufanikisha malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2050, hivyo ni muhimu vipaji vyao kuendelezwa na kupewa nafasi ya kukua.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Ayubu Sebabile, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mashindano hayo, amewataka wanafunzi kutumia vipaji vyao kubuni mawazo yatakayosaidia kuongeza uzalishaji wa chakula nchini.

Sebabile amesema ubunifu wa vijana unaweza kuchangia azma ya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa uzalishaji wa chakula barani Afrika na duniani.

Aidha, ameeleza matarajio yake ya kuona wanafunzi wakiwasilisha michoro yenye ujumbe unaoendana na malengo ya mashindano hayo, huku akibainisha kuwa washiriki wameandaliwa zawadi za kutambua juhudi na ubunifu wao.

Alisema washindi watano watakabidhiwa zawadi maalumu Oktoba 16, 2026, wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani yatakayofanyika jijini Tanga.

Naye msimamizi wa mashindano hayo kutoka FAO amesema lengo ni kuwajengea wanafunzi uelewa kuhusu kaulimbiu ya mwaka huu na kuwahamasisha kuitumia kama msingi wa michoro yao.

Amefafanua kuwa michoro hiyo inalenga kuonesha uhusiano kati ya ubunifu, chakula na lishe, pamoja na mchango wa masuala hayo katika kufanikisha malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2050.

Ameongeza kuwa kazi zote za washiriki zitapitiwa na wataalamu, kabla ya washindi watano kukabidhiwa zawadi katika kilele cha maadhimisho hayo Oktoba 16, 2026, jijini Tanga.

0 Hifadhi

Habari zinazohusiana

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

Top Stories · 20 Okt

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

Top Stories · 16 Okt

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

Top Stories · 16 Okt

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

Top Stories · 16 Okt

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Top Stories · 16 Okt

© 2026 Salamba TVMasharti ya matumiziSera ya faraghaSera ya marejeshoBeti kwa kuwajibika. Watu wazima 18+ pekee.

Shiriki kwa

Habari zinazohusiana

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

Top Stories · 20 Okt

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

Top Stories · 16 Okt

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

Top Stories · 16 Okt

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

Top Stories · 16 Okt

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Top Stories · 16 Okt

Zaidi kutoka

Top Stories →