Mwanamume mmoja nchini Uganda, anayetajwa kwa jina la Muhamud, anadaiwa kuwasha moto nyumba yake usiku wa Septemba 6, 2026, katika eneo la Kibenge, Wilaya ya Kasese, magharibi mwa nchi hiyo, wakati binti zake wawili, Amina na Shamila, walikuwa wamelala ndani.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, wasichana hao walikuwa wameacha Uislamu na kujiunga na Ukristo Agosti 26, 2026, hatua inayodaiwa kumkasirisha baba yao.
Inadaiwa kuwa kabla ya tukio hilo, Muhamud alikuwa amewaonya binti zake kwamba angechukua hatua kwa kile alichokitaja kuwa ni “kutimiza sheria ya Kiislamu.”
Hata hivyo, Amina na Shamila waliweza kujiokoa kwa kutoroka kupitia shimo walilodaiwa kutoboa ukutani. Moto huo uliteketeza nyumba yao pamoja na mali zilizokuwamo ndani, lakini wasichana hao walinusurika.
Akizungumzia tukio hilo, Amina amenukuliwa akisema kuwa moto huo uliteketeza makazi yao, lakini haukuweza kuteketeza imani yao.






