SalambaTV
NyumbaniHabariJamvikaRatibaRedio
  • Top Stories
  • Breaking News
  • Transfers
  • NBC Premier League
  • Match Highlights
  • Fixtures & Results
  • Standings & Tables
  • Tactical Analysis
NyumbaniHabariJamvikaRatibaRedio
SalambaTV
Ingia
Rudi nyumbani
Ingia

BWAWA LA MWAMBAZI LA SH BILIONI 2.1 KUTATUA CHANGAMOTO YA MAJI SUMBAWANGA

Salamba TV· Top Stories· 12 Oktoba 2026· 1 dakika za kusoma· 40 wasomaji
BWAWA LA MWAMBAZI LA SH BILIONI 2.1 KUTATUA CHANGAMOTO YA MAJI SUMBAWANGA

WANANCHI wa Kata ya Majengo, katika Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa, wanatarajia kupata nafuu ya upatikanaji wa maji kufuatia kukamilika kwa ujenzi wa Bwawa la Mwambazi lililogharimu Sh bilioni 2.1.

Mradi huo unalenga kuongeza upatikanaji wa maji na kupunguza changamoto ya mgao wa maji ambayo imekuwa ikiwaathiri wakazi wa eneo hilo katika shughuli zao za kila siku na kujipatia kipato.

Baadhi ya wananchi wa Kata ya Majengo wamesema kukamilika kwa bwawa hilo kumewapa matumaini ya kupata huduma ya maji kwa urahisi zaidi na kupunguza changamoto ambazo wamekuwa wakikabiliana nazo kutokana na mgao wa maji.

Akizungumzia mradi huo, Msimamizi wa Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Rukwa, Mhandisi Emanuel Nduiya, amesema ujenzi wa bwawa hilo umekamilika na lina ujazo wa lita milioni 741.

Amesema bwawa hilo linatarajiwa kusambaza maji katika zaidi ya kata saba za Manispaa ya Sumbawanga, hatua itakayosaidia kupanua wigo wa upatikanaji wa huduma hiyo kwa wananchi.

Kwa upande wake, Mbunge wa Sumbawanga Mjini, Aeshi Hilaly, amesema kukamilika kwa mradi huo ni hatua muhimu katika kukabiliana na changamoto ya kukatika kwa maji mara kwa mara katika maeneo husika.

Hilaly ameyasema hayo wakati wa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika jimbo hilo, ambapo amesisitiza umuhimu wa wananchi kushiriki katika kulinda miundombinu ya maji.

Amewataka wananchi kutunza miundombinu hiyo ili iweze kuendelea kutoa huduma kwa ufanisi na kuhakikisha uwekezaji huo unanufaisha kizazi cha sasa na kijacho.

0 Hifadhi

Habari zinazohusiana

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

Top Stories · 20 Okt

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

Top Stories · 16 Okt

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

Top Stories · 16 Okt

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

Top Stories · 16 Okt

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Top Stories · 16 Okt

© 2026 Salamba TVMasharti ya matumiziSera ya faraghaSera ya marejeshoBeti kwa kuwajibika. Watu wazima 18+ pekee.

Shiriki kwa

Habari zinazohusiana

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

Top Stories · 20 Okt

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

Top Stories · 16 Okt

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

Top Stories · 16 Okt

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

Top Stories · 16 Okt

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Top Stories · 16 Okt

Zaidi kutoka

Top Stories →