Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Mhe. Aswege Enock Kaminyoge, amezitaka kamati zote kuanzia ngazi ya serikali za mitaa hadi halmashauri kuhakikisha mikutano yao inafanyika kwa wakati kwa kuzingatia kalenda na ratiba zilizowekwa.
Mhe. Kaminyoge amesema utekelezaji wa ratiba hizo utasaidia kupunguza changamoto na migogoro kwa wananchi, hususan ile inayoweza kutatuliwa kupitia vikao na mikutano ya kiserikali.
Mkuu huyo wa Wilaya ametoa agizo hilo leo wakati akihutubia Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Mji wa Bunda, lililoketi kujadili taarifa za robo ya nne ya mwaka wa fedha 2025/2026.
Aidha, ameiagiza Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kuongeza juhudi za kusafisha mitaro na mifereji ya maji katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kukabiliana na athari zinazoweza kusababishwa na mvua za El Niño.
Kwa niaba ya Meneja wa TARURA Wilaya ya Bunda, Mhandisi Hamedi Munisi, amesema tayari wanaendelea na zoezi la kuzibua mitaro na kusafisha maeneo yenye uwezekano wa kuzuia mtiririko wa maji.






