Tume ya Ushindani (FCC) imewajengea uwezo wakufunzi wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (DPA) kuhusu utambuzi wa bidhaa bandia, ikiwa ni hatua ya kuongeza uelewa na kuimarisha mapambano dhidi ya bidhaa hizo nchini.
Kaimu Mkurugenzi wa Bidhaa Bandia wa FCC, Salvatore Chuwa, amesema wakufunzi hao watakuwa mabalozi wa kutoa elimu kwa wanafunzi na jamii kuhusu namna ya kutambua na kubaini bidhaa bandia.
Amesema mafunzo hayo yamewapa washiriki ujuzi wa kutofautisha bidhaa halisi na bandia kwa kuangalia alama za biashara, vifungashio, namba za usajili pamoja na viwango vinavyotolewa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).
FCC pamoja na washiriki wa mafunzo hayo wamesema wataendelea kushirikiana na vyuo na taasisi mbalimbali za elimu katika kuongeza uelewa wa umma na kupunguza usambazaji wa bidhaa bandia.
Wamesema bidhaa hizo zinaweza kuathiri uchumi na kuhatarisha afya na usalama wa watumiaji.






