SalambaTV
NyumbaniHabariJamvikaRatibaRedio
  • Top Stories
  • Breaking News
  • Transfers
  • NBC Premier League
  • Match Highlights
  • Fixtures & Results
  • Standings & Tables
  • Tactical Analysis
NyumbaniHabariJamvikaRatibaRedio
SalambaTV
Ingia
Rudi nyumbani
Ingia

MAKADA WA CCM RUVUMA WANUFAIKA NA MAFUNZO YA ITIKADI YA CHAMA

Salamba TV· Top Stories· 12 Oktoba 2026· 1 dakika za kusoma· 42 wasomaji
MAKADA WA CCM RUVUMA WANUFAIKA NA MAFUNZO YA ITIKADI YA CHAMA

MAKADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Ruvuma wameanza mafunzo maalumu ya itikadi ya chama hicho, yanayolenga kuimarisha uelewa wao kuhusu misingi, maadili na masuala mbalimbali yanayohusu chama.

Mafunzo hayo yameanza Oktoba 9, 2026, na yanatarajiwa kuhitimishwa Oktoba 25, mwaka huu, yakihusisha makada kutoka wilaya mbalimbali za Mkoa wa Ruvuma, ikiwa ni sehemu ya programu ya mafunzo yanayoendeshwa kwa wanachama wa CCM nchini kote.

Akizungumza kwa niaba ya wanachama wanaoshiriki mafunzo hayo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma, Oddo Kiliani Mwisho, amesema wamepokea mafunzo hayo kwa furaha, akibainisha kuwa baadhi ya wanachama wamekuwa wakikosa fursa za kupata mafunzo ya aina hiyo kwa muda mrefu.

Mwisho, ambaye anashiriki mafunzo hayo kama mwanafunzi katika darasa lililopo Kata ya Mjimwema, Wilaya ya Songea Mjini, ameipongeza CCM kwa kuandaa programu hiyo inayolenga kuwajengea wanachama uelewa mpana kuhusu itikadi na masuala ya chama.

Aidha, amempongeza Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwezesha mafunzo hayo kufanyika katika maeneo mbalimbali nchini, huku akimpongeza Mkuu wa Idara ya Itikadi na Uenezi wa CCM, Kenani Laban Kihongosi, kwa kuratibu mafunzo hayo na maandalizi ya walimu wanaohusika na utoaji wake.

Kwa upande wake, Mratibu wa mafunzo hayo mkoani Ruvuma, Edna Lameck, ambaye ni afisa wa Idara ya Itikadi na Uenezi kutoka Makao Makuu ya CCM, ametembelea madarasa mbalimbali yanayotoa mafunzo hayo ili kufuatilia utekelezaji wake.

Lameck amesema ameridhishwa na namna mafunzo hayo yanavyotolewa kwa makada wanaoshiriki katika madarasa mbalimbali mkoani humo.

Mafunzo hayo yanatarajiwa kuhitimishwa Oktoba 25, 2026, yakiwa na lengo la kuimarisha uwezo wa viongozi, makada na wanachama wa CCM katika kuelewa itikadi, misingi na masuala ya kisiasa yanayohusu chama hicho.

0 Hifadhi

Habari zinazohusiana

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

Top Stories · 20 Okt

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

Top Stories · 16 Okt

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

Top Stories · 16 Okt

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

Top Stories · 16 Okt

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Top Stories · 16 Okt

© 2026 Salamba TVMasharti ya matumiziSera ya faraghaSera ya marejeshoBeti kwa kuwajibika. Watu wazima 18+ pekee.

Shiriki kwa

Habari zinazohusiana

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

Top Stories · 20 Okt

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

Top Stories · 16 Okt

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

Top Stories · 16 Okt

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

Top Stories · 16 Okt

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Top Stories · 16 Okt

Zaidi kutoka

Top Stories →