SalambaTV
NyumbaniHabariJamvikaRatibaRedio
  • Top Stories
  • Breaking News
  • Transfers
  • NBC Premier League
  • Match Highlights
  • Fixtures & Results
  • Standings & Tables
  • Tactical Analysis
NyumbaniHabariJamvikaRatibaRedio
SalambaTV
Ingia
Rudi nyumbani
Ingia

MASAUNI AAGIZA MIFUMO ENDELEVU YA USIMAMIZI WA TAKA DAR ES SALAAM

Salamba TV· Top Stories· 12 Oktoba 2026· 2 dakika za kusoma· 29 wasomaji
MASAUNI AAGIZA MIFUMO ENDELEVU YA USIMAMIZI WA TAKA DAR ES SALAAM

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhandisi Hamad Yussuf Masauni, amezitaka mamlaka za Jiji la Dar es Salaam kuimarisha mifumo ya ukusanyaji na utunzaji wa taka, kudhibiti uchafuzi wa mazingira na kuweka mikakati ya kupunguza athari zinazoweza kusababishwa na mvua za El Niño.

Masauni amesema usafi wa jiji unapaswa kuwa sehemu ya majukumu ya kila siku ya taasisi na mamlaka zinazohusika na usimamizi wa mazingira, badala ya kusubiri maagizo kutoka kwa viongozi wa ngazi za juu.

Ameeleza kuwa Dar es Salaam ni taswira ya nchi, hivyo viongozi katika ngazi zote wanapaswa kuhakikisha usafi na utunzaji wa mazingira vinaimarishwa na kuzingatiwa wakati wote.

Waziri huyo ametoa maelekezo hayo Oktoba 11, 2026, wakati wa ziara ya kukagua shughuli za usafi na hatua za uhifadhi wa mazingira katika Mto Ng’ombe, uliopo Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Amesema pamoja na changamoto za upangaji wa makazi zinazojitokeza katika baadhi ya maeneo ya jiji, mamlaka husika zinapaswa kuweka mikakati madhubuti ya kuzuia utupaji holela wa taka na kuhakikisha taka zinakusanywa na kutunzwa kwa utaratibu unaofaa.

Masauni amesisitiza kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais haitaruhusu uzembe katika utekelezaji wa majukumu ya usafi na uhifadhi wa mazingira, akizitaka taasisi, halmashauri na viongozi wa mkoa na wilaya kusimamia ipasavyo utekelezaji wa wajibu huo.

Aidha, amebainisha kuwa taka zinaweza kuwa rasilimali yenye thamani ya kiuchumi na chanzo cha ajira kwa wananchi endapo zitakusanywa, kutenganishwa na kuchakatwa kwa njia zinazofaa.

Kutokana na hilo, amezitaka mamlaka zinazohusika kuboresha mifumo ya usimamizi wa taka ili kuongeza matumizi yake yenye tija na kupunguza athari zinazoweza kujitokeza kutokana na utupaji usiofaa, ikiwemo kuhatarisha afya za wananchi na kuharibu mazingira.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule, amesema wilaya hiyo inaendelea kutekeleza kampeni za kuhamasisha wananchi kushiriki katika usafi na utunzaji wa mazingira.

Mtambule amesema wananchi wanaoishi karibu na Mto Ng’ombe wameelekezwa kuhama katika maeneo hayo kutokana na hatari zinazoweza kusababishwa na mvua, huku zoezi la kubomoa nyumba zilizopo katika maeneo husika likiwa limeanza.

Ameongeza kuwa shughuli za ukusanyaji na usimamizi wa taka zinaendelea, sambamba na juhudi za kuhamasisha jamii kushiriki katika kulinda mazingira na kuzuia uchafuzi.

Amesisitiza kuwa ushirikiano kati ya viongozi na wananchi ni muhimu katika kuhakikisha jiji linakuwa safi na salama, huku hatua za kudhibiti uchafuzi na kupunguza athari za mvua zikiendelea kutekelezwa kwa ufanisi

0 Hifadhi

Habari zinazohusiana

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

Top Stories · 20 Okt

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

Top Stories · 16 Okt

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

Top Stories · 16 Okt

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

Top Stories · 16 Okt

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Top Stories · 16 Okt

© 2026 Salamba TVMasharti ya matumiziSera ya faraghaSera ya marejeshoBeti kwa kuwajibika. Watu wazima 18+ pekee.

Shiriki kwa

Habari zinazohusiana

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

Top Stories · 20 Okt

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

Top Stories · 16 Okt

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

Top Stories · 16 Okt

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

Top Stories · 16 Okt

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Top Stories · 16 Okt

Zaidi kutoka

Top Stories →