SalambaTV
NyumbaniHabariJamvikaRatibaRedio
  • Top Stories
  • Breaking News
  • Transfers
  • NBC Premier League
  • Match Highlights
  • Fixtures & Results
  • Standings & Tables
  • Tactical Analysis
NyumbaniHabariJamvikaRatibaRedio
SalambaTV
Ingia
Rudi nyumbani
Ingia

MKAZI WA BUNJU AKABILIWA NA MASHTAKA YA KUMUUA MKEWE

Salamba TV· Top Stories· 16 Oktoba 2026· 1 dakika za kusoma· 70 wasomaji
MKAZI WA BUNJU AKABILIWA NA MASHTAKA YA KUMUUA MKEWE

Mkazi wa Bunju A, Dar es Salaam, Laurence Kweka (48), amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni akikabiliwa na shtaka la kumuua mkewe, Jane Urassa.

Kweka amesomewa shtaka hilo leo, Oktoba 15, 2026, na Wakili wa Serikali, Harrison Lukos, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Kemilembe Josiah.

Kwa mujibu wa maelezo ya shtaka, mshtakiwa anadaiwa kumuua mkewe Oktoba Mosi mwaka huu, katika eneo la Bunju A, Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Kabla ya kusomewa shtaka hilo, mshtakiwa alielezwa kuwa hatakiwi kujibu chochote mahakamani kwa kuwa shauri hilo bado halijafikia hatua ya kusikilizwa kwa ushahidi.

Hakimu Josiah alimweleza Kweka kuwa kosa la mauaji analotuhumiwa nalo halina dhamana kwa mujibu wa sheria.

Aidha, mahakama ilibainisha kuwa haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo la mauaji, hivyo mshtakiwa ataendelea kusalia mahabusu wakati uchunguzi ukiendelea, kabla ya shauri hilo kupelekwa Mahakama Kuu kwa hatua zinazofuata.

Mahakama pia ilieleza kuwa shauri hilo litaendeshwa kwa njia ya mtandao huku mshtakiwa akiwa mahabusu.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 29, 2026, kwa ajili ya kutajwa tena.

0 Hifadhi

Habari zinazohusiana

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

Top Stories · 20 Okt

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

Top Stories · 16 Okt

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

Top Stories · 16 Okt

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

Top Stories · 16 Okt

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Top Stories · 16 Okt

© 2026 Salamba TVMasharti ya matumiziSera ya faraghaSera ya marejeshoBeti kwa kuwajibika. Watu wazima 18+ pekee.

Shiriki kwa

Habari zinazohusiana

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

Top Stories · 20 Okt

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

Top Stories · 16 Okt

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

Top Stories · 16 Okt

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

Top Stories · 16 Okt

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Top Stories · 16 Okt

Zaidi kutoka

Top Stories →