SalambaTV
NyumbaniHabariJamvikaRatibaRedio
  • Top Stories
  • Breaking News
  • Transfers
  • NBC Premier League
  • Match Highlights
  • Fixtures & Results
  • Standings & Tables
  • Tactical Analysis
NyumbaniHabariJamvikaRatibaRedio
SalambaTV
Ingia
Rudi nyumbani
Ingia

MWENGE WA UHURU WAKAGUA NA KUZINDUA MIRADI YA MAENDELEO KWELA

Salamba TV· Top Stories· 12 Oktoba 2026· 1 dakika za kusoma· 31 wasomaji
MWENGE WA UHURU WAKAGUA NA KUZINDUA MIRADI YA MAENDELEO KWELA

Mwenge wa Uhuru umeendelea kuhamasisha maendeleo nchini kwa kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya kijamii katika Jimbo la Kwela, Wilaya ya Sumbawanga, Mkoa wa Rukwa, huku wananchi wakihimizwa kuendelea kulinda amani na mshikamano ili kuweka mazingira bora ya utekelezaji wa miradi hiyo.

Katika ziara yake iliyofanyika Kata ya Laela, Mwenge wa Uhuru umepitia miradi inayohusisha sekta za elimu, afya na miundombinu, ikiwemo shule ya sekondari, zahanati na daraja, pamoja na shughuli za ujenzi wa barabara.

Miradi hiyo inalenga kuboresha huduma za kijamii na kuongeza ustawi wa wananchi, sambamba na kuimarisha uwajibikaji katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo.

Akizungumza Oktoba 10, 2026, katika Kata ya Laela, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Wazo Mwang’onda, amesema maendeleo yanayoendelea kutekelezwa nchini yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na uwepo wa amani na utulivu.

Amewataka wananchi wa Mkoa wa Rukwa kuendelea kudumisha amani, akieleza kuwa maendeleo endelevu yanahitaji ushirikiano, mshikamano na mazingira yenye utulivu.

Naye Mbunge wa Jimbo la Kwela, ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu, ameishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kupeleka miradi ya maendeleo mkoani Rukwa, hususan katika Jimbo la Kwela.

Amesema utekelezaji wa miradi hiyo ni sehemu ya juhudi za kuboresha huduma kwa wananchi na kuchochea maendeleo katika maeneo mbalimbali ya jimbo hilo.

0 Hifadhi

Habari zinazohusiana

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

Top Stories · 20 Okt

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

Top Stories · 16 Okt

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

Top Stories · 16 Okt

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

Top Stories · 16 Okt

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Top Stories · 16 Okt

© 2026 Salamba TVMasharti ya matumiziSera ya faraghaSera ya marejeshoBeti kwa kuwajibika. Watu wazima 18+ pekee.

Shiriki kwa

Habari zinazohusiana

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

Top Stories · 20 Okt

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

Top Stories · 16 Okt

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

Top Stories · 16 Okt

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

Top Stories · 16 Okt

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Top Stories · 16 Okt

Zaidi kutoka

Top Stories →