Waziri Mkuu wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, ametembelea Vatican City jijini Roma, Italia, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kando ya Mkutano wa Kimataifa wa Afya Moja na Mifumo ya Chakula na Kilimo uliofanyika katika Makao Makuu ya Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO).
Akiwa Vatican City, Dkt. Mwigulu amekutana na Mkuu wa Itifaki wa Sekretarieti ya Nchi ya Vatican, Monsinyori Javier Domingo Fernández González.
Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu pia ametembelea maeneo mbalimbali ya kihistoria na kiutamaduni yaliyopo Vatican City, ambayo yana umuhimu mkubwa katika historia ya Kanisa Katoliki duniani.






