SalambaTV
NyumbaniHabariJamvikaRatibaRedio
  • Top Stories
  • Breaking News
  • Transfers
  • NBC Premier League
  • Match Highlights
  • Fixtures & Results
  • Standings & Tables
  • Tactical Analysis
NyumbaniHabariJamvikaRatibaRedio
SalambaTV
Ingia
Rudi nyumbani
Ingia

NMB, TAMISA KUSHIRIKIANA KUKUZA MITAJI YA WATOA HUDUMA MIGODINI

Salamba TV· Top Stories· 12 Oktoba 2026· 1 dakika za kusoma· 28 wasomaji
NMB, TAMISA KUSHIRIKIANA KUKUZA MITAJI YA WATOA HUDUMA MIGODINI

BENKI ya NMB na Chama cha Wasambazaji wa Bidhaa na Huduma katika Sekta ya Madini Tanzania (TAMISA) zimesaini makubaliano ya ushirikiano ya miaka mitano yanayolenga kuwawezesha wanachama wa chama hicho kupata huduma za kifedha, elimu ya fedha, ushauri wa biashara na mafunzo ya kuwajengea uwezo.

Kupitia makubaliano hayo, NMB itapokea na kutathmini miradi inayowasilishwa na wanachama wa TAMISA, huku miradi itakayokidhi vigezo vya mikopo ikipata fursa ya kufadhiliwa na benki hiyo.

Ushirikiano huo pia unalenga kuongeza uwezo wa watoa huduma katika sekta ya madini kusimamia fedha, kukuza biashara zao na kutekeleza kandarasi zinazotokana na fursa mbalimbali katika mnyororo wa thamani wa madini.

Akizungumzia ushirikiano huo, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi, amesema ukosefu wa mtaji umekuwa miongoni mwa changamoto kubwa zinazowakabili watoa huduma wengi wanaofanya shughuli zao katika migodi.

Mponzi amesema NMB imeendelea kuimarisha huduma zake za kifedha kwa sekta ya madini, ikiwemo kuanzisha dawati maalumu kwa ajili ya kuwahudumia wasambazaji na watoa huduma wanaoshiriki katika sekta hiyo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Masoko na Uwekezaji ya TAMISA, Dk. Sebastian Ndege, amesema makubaliano hayo yatakuwa na mchango muhimu katika kuwawezesha wanachama kupata mitaji, kuongeza uwezo wa kushindania zabuni na kutumia fursa za biashara zinazopatikana katika sekta ya madini.

Ameeleza kuwa upatikanaji wa huduma za kifedha pamoja na mafunzo ya biashara utawasaidia wanachama wa TAMISA kuimarisha shughuli zao na kushiriki kwa ufanisi zaidi katika mnyororo wa thamani wa sekta ya madini nchini.

0 Hifadhi

Habari zinazohusiana

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

Top Stories · 20 Okt

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

Top Stories · 16 Okt

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

Top Stories · 16 Okt

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

Top Stories · 16 Okt

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Top Stories · 16 Okt

© 2026 Salamba TVMasharti ya matumiziSera ya faraghaSera ya marejeshoBeti kwa kuwajibika. Watu wazima 18+ pekee.

Shiriki kwa

Habari zinazohusiana

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

Top Stories · 20 Okt

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

Top Stories · 16 Okt

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

Top Stories · 16 Okt

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

Top Stories · 16 Okt

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Top Stories · 16 Okt

Zaidi kutoka

Top Stories →