Cristiano Ronaldo ameweka rekodi ya kufunga mabao dhidi ya klabu 159 tofauti katika historia ya soka.
Nyota huyo wa Ureno ana nafasi ya kuweka rekodi mpya ya dunia iwapo atafanikiwa kufunga bao dhidi ya klabu ya Al-Diraiyah, hatua itakayomfanya kuwa mchezaji wa kwanza katika historia kufunga mabao dhidi ya klabu 160 tofauti.
Ronaldo anaendelea kuandika historia katika soka la dunia kupitia uwezo wake wa kufunga mabao dhidi ya wapinzani mbali.






