SalambaTV
NyumbaniHabariJamvikaRatibaRedio
  • Top Stories
  • Breaking News
  • Transfers
  • NBC Premier League
  • Match Highlights
  • Fixtures & Results
  • Standings & Tables
  • Tactical Analysis
NyumbaniHabariJamvikaRatibaRedio
SalambaTV
Ingia
Rudi nyumbani
Ingia

SANGU AIPONGEZA SERIKALI KWA KUBORESHA HUDUMA ZA HIFADHI YA JAMII

Salamba TV· Top Stories· 15 Oktoba 2026· 2 dakika za kusoma· 52 wasomaji
SANGU AIPONGEZA SERIKALI KWA KUBORESHA HUDUMA ZA HIFADHI YA JAMII

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu, ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuimarisha mifuko ya hifadhi ya jamii, ikiwemo kuboresha ulipaji wa mafao kwa wanachama na wastaafu kwa wakati.

Sangu ametoa pongezi hizo Oktoba 12, 2026, mjini Sumbawanga mkoani Rukwa, wakati wa uzinduzi wa semina za kuwaandaa wastaafu watarajiwa wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwa kipindi cha mwaka 2026/2028.

Akizungumza katika hafla hiyo, Waziri Sangu amesema hatua zilizochukuliwa na Serikali zimewezesha kuimarika kwa mifuko ya hifadhi ya jamii, ikiwemo kuendelea kulipa madeni inayodaiwa na mifuko hiyo, kuhakikisha mafao yanapatikana kwa wakati na kuboresha kiwango cha chini cha pensheni kwa wastaafu.

Amesema kiwango cha chini cha pensheni kwa wastaafu kimefikia Shilingi 250,000 kwa mwezi, akieleza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali kuboresha maisha na ustawi wa wastaafu baada ya kumaliza utumishi wao.

Waziri huyo pia ameipongeza PSSSF kwa kuandaa semina zinazolenga kuwapa watumishi wanaokaribia kustaafu maarifa na maandalizi muhimu ya kukabiliana na maisha baada ya utumishi wa umma.

Amesema mafunzo hayo ni muhimu katika kuwasaidia wastaafu watarajiwa kupanga maisha yao ya baadaye na kutumia vizuri mafao watakayopata baada ya kustaafu.

Semina hizo zinatarajiwa kufanyika katika mikoa ya Mwanza, Arusha, Dar es Salaam na Dodoma, pamoja na Unguja kwa upande wa Zanzibar. Sangu ameitaka PSSSF kuhakikisha programu hiyo inaendelea kutolewa ili kuwafikia watumishi wengi zaidi wanaokaribia kustaafu.

Akizungumzia kaulimbiu ya mfuko huo, “Tunalipa Jana,” Sangu amesema inaakisi dhamira ya PSSSF ya kuhakikisha mafao ya wanachama yanalipwa kwa wakati, huku akiwahimiza wastaafu watarajiwa kuwa na imani na mfuko huo.

Ameeleza kuwa utekelezaji wa kaulimbiu hiyo unaonesha umuhimu wa maboresho yaliyofanywa katika mifumo ya utoaji wa huduma kwa wanachama na wastaafu.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Makongoro Nyerere, ameitaka PSSSF kuendelea kuimarisha uhusiano na wastaafu na kuhakikisha mafao yao yanalipwa kwa usahihi na kwa wakati.

Nyerere amesema mfuko huo unapaswa kuendelea kuwa nguzo ya uhakika na faraja kwa watumishi wanapohitimisha utumishi wao, kwa kuhakikisha wanapata stahiki zao bila usumbufu usio wa lazima.

0 Hifadhi

Habari zinazohusiana

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

Top Stories · 20 Okt

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

Top Stories · 16 Okt

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

Top Stories · 16 Okt

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

Top Stories · 16 Okt

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Top Stories · 16 Okt

© 2026 Salamba TVMasharti ya matumiziSera ya faraghaSera ya marejeshoBeti kwa kuwajibika. Watu wazima 18+ pekee.

Shiriki kwa

Habari zinazohusiana

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

Top Stories · 20 Okt

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

Top Stories · 16 Okt

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

Top Stories · 16 Okt

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

Top Stories · 16 Okt

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Top Stories · 16 Okt

Zaidi kutoka

Top Stories →