SalambaTV
NyumbaniHabariJamvikaRatibaRedio
  • Top Stories
  • Breaking News
  • Transfers
  • NBC Premier League
  • Match Highlights
  • Fixtures & Results
  • Standings & Tables
  • Tactical Analysis
NyumbaniHabariJamvikaRatibaRedio
SalambaTV
Ingia
Rudi nyumbani
Ingia

SERIKALI: SERA YA MNYORORO WA UGAVI 2025 FURSA KWA WANAWAKE NA VIJANA

Salamba TV· Top Stories· 2 Oktoba 2026· 1 dakika za kusoma· 25 wasomaji
SERIKALI: SERA YA MNYORORO WA UGAVI 2025 FURSA KWA WANAWAKE NA VIJANA

Serikali imesema Sera ya Taifa ya Usimamizi wa Mnyororo wa Ugavi ya mwaka 2025 ni fursa kwa Watanzania, hususan wanawake, vijana na makundi mengine maalumu, kushiriki zaidi katika zabuni na shughuli za usambazaji wa bidhaa na huduma kwa Serikali.

Kaimu Kamishna wa Sera za Ununuzi wa Umma katika Wizara ya Fedha, Alex Haraba, amesema sera hiyo inalenga kuongeza matumizi ya bidhaa, huduma na malighafi zinazozalishwa nchini, hatua inayotarajiwa kupanua soko la wazawa, kuchochea ajira na kuongeza uwekezaji.

Akizungumza katika mafunzo kwa wahariri wa vyombo vya habari na wamiliki wa mitandao ya kijamii, Haraba amesema sehemu kubwa ya mapato ya Serikali hutumika katika ununuzi wa bidhaa na huduma, hivyo Watanzania wanapaswa kuona matumizi hayo kama fursa ya kushiriki katika shughuli za kiuchumi.

Kwa upande wake, Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Maige Mwasimba, amesema mnyororo wa ugavi unahusisha hatua mbalimbali, kuanzia upangaji wa mahitaji, ununuzi, upokeaji, uhifadhi, usambazaji, matumizi hadi uondoshaji wa mali.

Amesema tofauti na awali ambapo msisitizo mkubwa uliwekwa kwenye ununuzi, sera ya sasa imepanua wigo kwa kuzingatia hatua zote za mnyororo wa ugavi.

Sera hiyo pia inalenga kuboresha ufanisi wa huduma za kijamii, ikiwemo afya, elimu, maji, umeme na miundombinu, kupitia matumizi bora ya rasilimali za umma.

Utekelezaji wa sera hiyo unalenga pia kuchangia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kwa kukuza uzalishaji wa ndani, sekta binafsi, viwanda, ajira na ushindani, huku matumizi ya Serikali yakitumika kuchochea ukuaji wa uchumi jumuishi.

0 Hifadhi

Habari zinazohusiana

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

Top Stories · 20 Okt

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

Top Stories · 16 Okt

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

Top Stories · 16 Okt

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

Top Stories · 16 Okt

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Top Stories · 16 Okt

© 2026 Salamba TVMasharti ya matumiziSera ya faraghaSera ya marejeshoBeti kwa kuwajibika. Watu wazima 18+ pekee.

Shiriki kwa

Habari zinazohusiana

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

Top Stories · 20 Okt

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

Top Stories · 16 Okt

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

Top Stories · 16 Okt

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

Top Stories · 16 Okt

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Top Stories · 16 Okt

Zaidi kutoka

Top Stories →