SalambaTV
NyumbaniHabariJamvikaRatibaRedio
  • Top Stories
  • Breaking News
  • Transfers
  • NBC Premier League
  • Match Highlights
  • Fixtures & Results
  • Standings & Tables
  • Tactical Analysis
NyumbaniHabariJamvikaRatibaRedio
SalambaTV
Ingia
Rudi nyumbani
Ingia

SERIKALI YAONGEZA KASI YA MIRADI YA MAJI VIJIJINI

Salamba TV· Top Stories· 12 Oktoba 2026· 1 dakika za kusoma· 41 wasomaji
SERIKALI YAONGEZA KASI YA MIRADI YA MAJI VIJIJINI

SERIKALI imesema imejipanga kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma ya maji safi, salama na ya kutosha, huku ikiweka mikakati ya kuharakisha utekelezaji wa miradi ya maji katika maeneo ambayo bado hayajafikiwa na huduma hiyo.

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, ameyasema hayo jijini Dodoma wakati wa kikao na Menejimenti ya Sekta ya Maji, akisisitiza umuhimu wa kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ili wananchi wanufaike na huduma ya maji kwa wakati.

Amesema mpango wa kusambaza maji katika vijiji ambavyo havina miundombinu ya huduma hiyo umeanza kutekelezwa, ambapo kwa sasa miradi inajengwa katika vijiji 400 kati ya vijiji 1,575 vilivyopangwa kufikiwa katika awamu mbalimbali.

Aweso amewataka wataalamu wa sekta hiyo kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi hiyo ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama.

Katika hatua nyingine, amesema ukaguzi wa miradi ya maji alioufanya umebaini changamoto zinazohitaji kutatuliwa kwa haraka, hivyo amewataka wataalamu wanaohusika kutoa majibu na mapendekezo ya suluhu ndani ya siku zisizozidi 30 ili kuwezesha wananchi kuanza kunufaika na miradi hiyo.

Kuhusu uhaba wa maji katika baadhi ya maeneo ya mijini, Waziri Aweso ameelekeza kuwekwa kwa mipango ya dharura itakayosaidia kupunguza changamoto hiyo na kuwawezesha wateja kupata huduma kwa unafuu.

Amesisitiza kuwa pale mgao wa maji unapolazimika kufanyika, unapaswa kuzingatia hali halisi ya upatikanaji wa maji na kupanga muda wa mgao unaotosheleza mahitaji ya wananchi.

Aidha, amesema maeneo yote yanayokabiliwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa maji yanajulikana, hivyo ametaka hatua madhubuti zichukuliwe ili kupata suluhu ya kudumu na kuboresha upatikanaji wa huduma hiyo kwa wananchi.

0 Hifadhi

Habari zinazohusiana

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

Top Stories · 20 Okt

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

Top Stories · 16 Okt

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

Top Stories · 16 Okt

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

Top Stories · 16 Okt

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Top Stories · 16 Okt

© 2026 Salamba TVMasharti ya matumiziSera ya faraghaSera ya marejeshoBeti kwa kuwajibika. Watu wazima 18+ pekee.

Shiriki kwa

Habari zinazohusiana

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

Top Stories · 20 Okt

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

Top Stories · 16 Okt

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

Top Stories · 16 Okt

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

Top Stories · 16 Okt

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Top Stories · 16 Okt

Zaidi kutoka

Top Stories →