SalambaTV
NyumbaniHabariJamvikaRatibaRedio
  • Top Stories
  • Breaking News
  • Transfers
  • NBC Premier League
  • Match Highlights
  • Fixtures & Results
  • Standings & Tables
  • Tactical Analysis
NyumbaniHabariJamvikaRatibaRedio
SalambaTV
Ingia
Rudi nyumbani
Ingia

TANESCO KAGERA YAHITIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA, WAFANYAKAZI WAZAWADIWA

Salamba TV· Top Stories· 12 Oktoba 2026· 1 dakika za kusoma· 44 wasomaji
TANESCO KAGERA YAHITIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA, WAFANYAKAZI WAZAWADIWA

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO), Mkoa wa Kagera, limehitimisha maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja kwa kufanya hafla maalumu iliyowakutanisha wafanyakazi na wateja, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha uhusiano na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma.

Katika maadhimisho hayo, TANESCO Kagera ilianza kwa kutoa elimu kupitia vituo vya redio kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na shirika hilo, pamoja na kuwaelimisha wananchi kuhusu tahadhari zinazopaswa kuchukuliwa wakati wa mvua za El Niño.

Baada ya shughuli hizo, wafanyakazi na wateja walikutana katika hafla iliyofanyika nje ya ofisi za TANESCO Mkoa wa Kagera, ambapo walishiriki chakula cha mchana na shughuli mbalimbali za kuadhimisha wiki hiyo, ikiwemo kukata keki.

Sambamba na hilo, wafanyakazi waliofanya vizuri katika kuwahudumia wateja walitambuliwa na kutunukiwa zawadi kama motisha ya kuendeleza utendaji bora. Wateja nao walipatiwa zawadi kwa kutambua mchango wao na kuonesha umuhimu wao katika shughuli za shirika hilo.

Akizungumza katika hafla hiyo, Meneja wa TANESCO Mkoa wa Kagera, Mhandisi Tumaini Nyari, amewapongeza wafanyakazi kwa juhudi zao katika kuwahudumia wateja na kuwasisitiza kudumisha utamaduni wa kutoa huduma bora, zenye ufanisi na zinazokidhi mahitaji ya wananchi.

Mhandisi Nyari amesema ni muhimu kwa wafanyakazi kuendelea kuboresha namna wanavyowahudumia wateja ili kuimarisha uhusiano na kuongeza imani ya wananchi kwa shirika hilo.

0 Hifadhi

Habari zinazohusiana

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

Top Stories · 20 Okt

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

Top Stories · 16 Okt

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

Top Stories · 16 Okt

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

Top Stories · 16 Okt

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Top Stories · 16 Okt

© 2026 Salamba TVMasharti ya matumiziSera ya faraghaSera ya marejeshoBeti kwa kuwajibika. Watu wazima 18+ pekee.

Shiriki kwa

Habari zinazohusiana

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

Top Stories · 20 Okt

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

Top Stories · 16 Okt

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

Top Stories · 16 Okt

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

Top Stories · 16 Okt

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Top Stories · 16 Okt

Zaidi kutoka

Top Stories →