SalambaTV
NyumbaniHabariJamvikaRatibaRedio
  • Top Stories
  • Breaking News
  • Transfers
  • NBC Premier League
  • Match Highlights
  • Fixtures & Results
  • Standings & Tables
  • Tactical Analysis
NyumbaniHabariJamvikaRatibaRedio
SalambaTV
Ingia
Rudi nyumbani
Ingia

TANZANIA NA BURUNDI ZAFUNGUA UKURASA MPYA WA USHIRIKIANO WA MAENDELEO YA KIMKAKATI.

Salamba TV· Top Stories· 1 Oktoba 2026· 2 dakika za kusoma· 23 wasomaji
TANZANIA NA BURUNDI ZAFUNGUA UKURASA MPYA WA USHIRIKIANO WA MAENDELEO YA KIMKAKATI.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Burundi, kwa pamoja zimekubaliana kuimarisha ushirikiano wa kimkakati katika maeneo ya mbalimbali ya kimaendeleo ikiwemo siasa na diplomasia, usalama, biashara, uwekezaji, miundombinu, nishati na maendeleo ya kijamii, hatua inayol

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Burundi, kwa pamoja zimekubaliana kuimarisha ushirikiano wa kimkakati katika maeneo ya mbalimbali ya kimaendeleo ikiwemo siasa na diplomasia, usalama, biashara, uwekezaji, miundombinu, nishati na maendeleo ya kijamii, hatua inayolenga kuongeza fursa za kiuchumi na kuboresha maisha ya wananchi wa nchi hizo mbili, ikiwa ni utekelezaji wa makubaliano ya Mkutano wa Sita wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirkiano uliofanyika mwaka 2021 Mkoani Kigoma.

Makubaliano hayo yamejadiliwa katika Mkutano wa Saba (7) wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (The 7th Joint Permanent Commission for Cooperation – JPC) ngazi ya Mawaziri, uliofanyika jijini Bujumbura nchini Burundi tarehe 30 Septemba, 2026

Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo umeongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo (Mb), ambapo pande hizo mbili zimejadili hatua za kuimarisha utekelezaji wa makubaliano ya ushirikiano na kutafuta fursa mpya za kukuza uhusiano wa Tanzania na Burundi.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mkutano huo, Waziri Kombo amesema Katika masuala ya kisiasa na kidiplomasia, nchi hizo zimejadili kuimarisha ushirikiano katika ulinzi na usalama, ikiwemo kudhibiti uhalifu wa majini katika Ziwa Tanganyika, kufanya operesheni na doria za pamoja katika maeneo ya mipakani, pamoja na kuzuia na kupambana na usafirishaji haramu wa binadamu.

Viongozi wengine walioshiriki mkutano huo kutoka nchini Tanzania ni pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia Masuala ya Afrika Mashariki, Bw. Charles Ngeleja Kadonya, Katibu Mkuu Wizara ya Kazi na Uwekezaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw. Mwalimu Khamis Suleiman, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Dkt. Franklin Jasson Rwezimula, Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Mhe. Gelasius Gaspar Byakanwa, na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ali Bujiku.


0 Hifadhi

Habari zinazohusiana

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

Top Stories · 20 Okt

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

Top Stories · 16 Okt

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

Top Stories · 16 Okt

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

Top Stories · 16 Okt

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Top Stories · 16 Okt

© 2026 Salamba TVMasharti ya matumiziSera ya faraghaSera ya marejeshoBeti kwa kuwajibika. Watu wazima 18+ pekee.

Shiriki kwa

Habari zinazohusiana

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

Top Stories · 20 Okt

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

Top Stories · 16 Okt

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

Top Stories · 16 Okt

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

Top Stories · 16 Okt

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Top Stories · 16 Okt

Zaidi kutoka

Top Stories →