SalambaTV
NyumbaniHabariJamvikaRatibaRedio
  • Top Stories
  • Breaking News
  • Transfers
  • NBC Premier League
  • Match Highlights
  • Fixtures & Results
  • Standings & Tables
  • Tactical Analysis
NyumbaniHabariJamvikaRatibaRedio
SalambaTV
Ingia
Rudi nyumbani
Ingia

TARURA YAWEKEZA SHILINGI BILIONI 2.76 KUBORESHA UCHUNGUZI WA UDONGO

Salamba TV· Top Stories· 12 Oktoba 2026· 2 dakika za kusoma· 33 wasomaji
TARURA YAWEKEZA SHILINGI BILIONI 2.76 KUBORESHA UCHUNGUZI WA UDONGO

Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imewekeza zaidi ya Shilingi bilioni 2.76 katika ununuzi wa vifaa vya kisasa vya uchunguzi wa udongo, hatua inayolenga kuimarisha usanifu wa barabara na madaraja, kuongeza uimara wa miundombinu na kupunguza gharama za ujenzi nchini.

Akizungumzia uwekezaji huo, Mtendaji Mkuu wa TARURA, Mhandisi Victor Seff, amesema wakala huo unasimamia ujenzi na matengenezo ya mtandao wa barabara za wilaya wenye urefu wa kilomita 144,149.18, unaojumuisha barabara za lami, changarawe na udongo.

Ameeleza kuwa katika mtandao huo, takribani kilomita 3,900 ni barabara za lami, zaidi ya kilomita 47,000 ni za changarawe na zaidi ya kilomita 92,000 ni za udongo, hali inayodhihirisha umuhimu wa kutumia teknolojia na tafiti za kitaalamu kuboresha ujenzi na matengenezo ya barabara hizo.

Mhandisi Seff amesema TARURA, kupitia Kitengo cha Tafiti na Udhibiti wa Ubora, hufanya uchunguzi wa udongo, hupima ubora wa kazi za ujenzi na kutafiti malighafi zinazoweza kutumika katika ujenzi wa barabara.

Amesema vifaa vipya vitaiwezesha taasisi hiyo kupata taarifa sahihi kuhusu sifa za udongo na uwezo wake wa kubeba mizigo, taarifa ambazo ni muhimu katika usanifu wa barabara na madaraja yenye uimara na yanayodumu kwa muda mrefu.

Aidha, uwekezaji huo unatarajiwa kuongeza ufanisi wa tafiti, kuimarisha uwezo wa wataalamu wa ndani na kubaini mbinu zinazoweza kupunguza gharama za ujenzi bila kuathiri viwango vya ubora vinavyotakiwa.

Kwa mujibu wa Mhandisi Seff, TARURA ina maabara kuu jijini Dodoma na maabara nyingine zaidi ya 15 katika mikoa mbalimbali nchini, zinazotoa huduma za kupima udongo, kuthibitisha ubora wa kazi za ujenzi na kuchunguza malighafi zinazopatikana katika maeneo ya miradi.

Amebainisha kuwa baadhi ya malighafi za ujenzi hupatikana mbali na maeneo ya utekelezaji wa miradi, hali inayoweza kuongeza gharama za usafirishaji. Kupitia tafiti za kitaalamu, TARURA huweza kubaini na kupima malighafi zinazopatikana karibu na miradi ili kuthibitisha kama zinafaa kutumika na zinakidhi viwango vinavyohitajika.

Amesisitiza kuwa huduma za maabara zina nafasi muhimu katika kuhakikisha udongo na malighafi zinazotumika zina ubora unaotakiwa, kazi za ujenzi zinatekelezwa kwa viwango vinavyokubalika na fedha zinazotumika katika miradi ya barabara zinatoa thamani iliyokusudiwa.

Katika kuimarisha matumizi ya miundombinu hiyo, Mhandisi Seff amewaalika makandarasi na wahandisi washauri wanaotekeleza miradi ya TARURA na taasisi nyingine kutumia huduma za maabara za wakala huo zilizopo Dodoma na katika mikoa mbalimbali nchini.

Amesema maabara hizo zina vifaa vinavyokidhi mahitaji ya sasa ya sekta ya ujenzi, huku wataalamu wa TARURA wakiwa wamepatiwa mafunzo yanayowawezesha kufanya uchunguzi na tafiti za udongo kwa ufanisi.

Ameongeza kuwa TARURA itaendelea kuongeza vifaa na kuimarisha maabara zilizopo mikoani ili kupanua huduma za upimaji na udhibiti wa ubora, na hivyo kuchangia ujenzi wa barabara na madaraja yenye viwango bora na uimara wa muda mrefu.

Uwekezaji huo ni sehemu ya juhudi za TARURA kutumia sayansi, teknolojia na tafiti za kitaalamu kuboresha usimamizi wa miundombinu ya barabara, kupunguza gharama zisizo za lazima na kuimarisha mtandao wa barabara unaochochea shughuli za kiuchumi na kijamii nchini.

0 Hifadhi

Habari zinazohusiana

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

Top Stories · 20 Okt

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

Top Stories · 16 Okt

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

Top Stories · 16 Okt

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

Top Stories · 16 Okt

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Top Stories · 16 Okt

© 2026 Salamba TVMasharti ya matumiziSera ya faraghaSera ya marejeshoBeti kwa kuwajibika. Watu wazima 18+ pekee.

Shiriki kwa

Habari zinazohusiana

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

Top Stories · 20 Okt

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

Top Stories · 16 Okt

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

Top Stories · 16 Okt

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

Top Stories · 16 Okt

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Top Stories · 16 Okt

Zaidi kutoka

Top Stories →