SalambaTV
NyumbaniHabariJamvikaRatibaRedio
  • Top Stories
  • Breaking News
  • Transfers
  • NBC Premier League
  • Match Highlights
  • Fixtures & Results
  • Standings & Tables
  • Tactical Analysis
NyumbaniHabariJamvikaRatibaRedio
SalambaTV
Ingia
Rudi nyumbani
Ingia

TEKNOLOJIA NA AKILI UNDE KUIMARISHA UENDESHAJI WA SACCOS AFRIKA

Salamba TV· Top Stories· 16 Oktoba 2026· 2 dakika za kusoma· 78 wasomaji
TEKNOLOJIA NA AKILI UNDE KUIMARISHA UENDESHAJI WA SACCOS AFRIKA

Matumizi ya teknolojia za kidijitali na Akili Unde (AI) yanatajwa kuwa miongoni mwa suluhisho muhimu katika kuboresha usimamizi, kuongeza ufanisi na kuimarisha utoaji wa huduma katika Vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS) barani Afrika.

Hayo yameelezwa Oktoba 14, 2026, jijini Dar es Salaam na Mrajis wa Vyama vya Ushirika Tanzania ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Dk. Benson Ndiege, akizungumzia mijadala inayofanyika katika Kongamano la Kimataifa la Vyama vya Akiba na Mikopo barani Afrika.

Dk. Ndiege amesema matumizi ya teknolojia ni miongoni mwa ajenda muhimu zinazojadiliwa katika Mkutano Mkuu wa 26 wa SACCO unaofanyika nchini Tanzania, ambapo wataalamu kutoka ndani na nje ya nchi wanabadilishana mawazo kuhusu namna mifumo ya kidijitali inavyoweza kuboresha shughuli za vyama vya ushirika na kuongeza ushiriki wa wananchi.

Ameeleza kuwa mijadala hiyo inalenga kuweka mapendekezo na maazimio ya pamoja yatakayovisaidia vyama vya ushirika kutumia teknolojia kutatua changamoto za kiutendaji na kuboresha huduma kwa wanachama wake.

Kwa mujibu wa Dk. Ndiege, matumizi ya mifumo ya kisasa yanaweza kurahisisha utunzaji wa kumbukumbu, kupunguza hatari ya kupotea kwa taarifa na kuongeza ufanisi katika usimamizi wa shughuli za kila siku za SACCOS.

Ameongeza kuwa kongamano hilo ni fursa muhimu kwa washiriki kujifunza kutoka kwa wenzao kuhusu maendeleo ya kiteknolojia na namna ya kuyatumia kukabiliana na mahitaji ya sekta ya ushirika katika kipindi hiki cha mabadiliko ya kidijitali.

Mbali na teknolojia, Dk. Ndiege amesema washiriki wanajadili pia masuala ya utawala bora, usimamizi wa vyama, matumizi ya takwimu katika kufanya maamuzi na namna ya kuongeza ushiriki wa vijana na wanawake katika sekta ya ushirika.

Amesisitiza kuwa matumizi sahihi ya takwimu ni muhimu katika kufanya maamuzi yenye tija, huku mifumo madhubuti ya usimamizi ikitarajiwa kuimarisha uwajibikaji, uwazi na ufanisi katika uendeshaji wa SACCOS.

Aidha, amesema vijana na wanawake ni miongoni mwa makundi yanayopewa kipaumbele katika mafunzo na mijadala ya mkutano huo kutokana na mchango wao katika kukuza uchumi na kuendeleza sekta ya ushirika.

Ameeleza kuwa kuwawezesha makundi hayo pamoja na kuimarisha matumizi ya teknolojia kutasaidia kupanua wigo wa wananchi wanaopata huduma za kifedha kupitia vyama vya akiba na mikopo.

Kongamano hilo lililoanza Oktoba 11, 2026, linatarajiwa kuhitimishwa Oktoba 16, mwaka huu, likiwa limejumuisha mafunzo, mijadala na ubadilishanaji wa uzoefu kuhusu usimamizi na maendeleo ya SACCOS barani Afrika.

0 Hifadhi

Habari zinazohusiana

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

Top Stories · 20 Okt

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

Top Stories · 16 Okt

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

Top Stories · 16 Okt

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

Top Stories · 16 Okt

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Top Stories · 16 Okt

© 2026 Salamba TVMasharti ya matumiziSera ya faraghaSera ya marejeshoBeti kwa kuwajibika. Watu wazima 18+ pekee.

Shiriki kwa

Habari zinazohusiana

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

Top Stories · 20 Okt

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

Top Stories · 16 Okt

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

Top Stories · 16 Okt

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

Top Stories · 16 Okt

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Top Stories · 16 Okt

Zaidi kutoka

Top Stories →