SalambaTV
NyumbaniHabariJamvikaRatibaRedio
  • Top Stories
  • Breaking News
  • Transfers
  • NBC Premier League
  • Match Highlights
  • Fixtures & Results
  • Standings & Tables
  • Tactical Analysis
NyumbaniHabariJamvikaRatibaRedio
SalambaTV
Ingia
Rudi nyumbani
Ingia

TIE NA VODACOM KUIMARISHA MAFUNZO YA WALIMU KUPITIA TEKNOLOJIA

Salamba TV· Top Stories· 12 Oktoba 2026· 2 dakika za kusoma· 28 wasomaji
TIE NA VODACOM KUIMARISHA MAFUNZO YA WALIMU KUPITIA TEKNOLOJIA

Maelfu ya walimu nchini wanatarajiwa kunufaika na fursa za mafunzo endelevu ya kitaaluma kupitia teknolojia ya kidijitali, katika juhudi za kuongeza ufanisi wa ufundishaji, kuboresha ufaulu wa wanafunzi na kuchangia maendeleo ya taifa kupitia elimu.

Mpango huo unatekelezwa kupitia ushirikiano kati ya Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE) na Vodacom Tanzania Foundation, kwa lengo la kuimarisha Programu ya Mafunzo Endelevu ya Walimu Kazini (TCPD/MEWAKA), inayotumia Mfumo wa Usimamizi wa Kujifunza (LMS) pamoja na Vituo vya Rasilimali za Walimu (TRC).

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi na makabidhiano ya Kituo cha Rasilimali za Walimu kilichojengwa katika Shule ya Msingi Naurei, Wilaya ya Arumeru, Mkuu wa Wilaya hiyo, Neema Lugangira, amesema uwekezaji katika maendeleo ya walimu ni hatua muhimu katika kuboresha ubora wa elimu nchini.

Kituo hicho ni cha kwanza kati ya vituo 50 vinavyotarajiwa kujengwa nchini kwa lengo la kuwawezesha walimu kupata maarifa mapya na kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) katika shughuli zao za ufundishaji.

Lugangira amesema ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi katika kuboresha miundombinu, teknolojia na mifumo ya kujifunzia unatoa fursa kwa walimu kujiendeleza kitaaluma na kuongeza uwezo wa wanafunzi kufikia malengo yao ya kielimu.

Amesema tathmini ya mahitaji ya programu ya TCPD/MEWAKA, iliyohusisha Vituo vya Rasilimali za Walimu 178, walimu 350 na wadau mbalimbali, imeonesha kuwa walimu wengi wana nia ya kujifunza na kutumia teknolojia katika kuendeleza taaluma zao.

Kwa mujibu wa tathmini hiyo, asilimia 99 ya walimu waliohusishwa walikuwa wanaifahamu mifumo ya LMS, huku asilimia 71 wakiwa na uelewa wa msingi wa matumizi ya TEHAMA.

Hata hivyo, amesema upatikanaji mdogo wa vifaa vya TEHAMA, kompyuta, huduma za intaneti na usaidizi wa kiufundi bado ni miongoni mwa changamoto zinazozuia walimu kutumia kikamilifu mifumo hiyo, hususan katika maeneo ya vijijini.

Lugangira amesisitiza kuwa mafanikio ya programu hiyo yanahitaji uwekezaji endelevu katika vifaa, huduma za intaneti na mafunzo ya vitendo yatakayowawezesha walimu kutumia teknolojia kwa ufanisi.

Aidha, ameipongeza Vodacom Tanzania Foundation kwa kushiriki katika kuimarisha sekta ya elimu na kuzitaka taasisi nyingine za sekta binafsi kuunga mkono juhudi za kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Foundation, Zuweina Farah, amesema uwekezaji katika maendeleo ya walimu ni njia muhimu ya kuboresha mfumo wa elimu na kuimarisha uchumi wa kidijitali nchini.

Farah amesema walimu wanapopata fursa za kujiendeleza kitaaluma na kutumia teknolojia ipasavyo, manufaa yake huonekana kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla.

Ameeleza kuwa kupitia ushirikiano na TIE, walimu wanaotumia mtandao wa Vodacom wanaweza kupata huduma za Mfumo wa Usimamizi wa Kujifunza (LMS) bila kutozwa gharama za data, hatua inayolenga kupunguza vikwazo vya upatikanaji wa maudhui ya mafunzo.

Amesema mpango huo unalenga kuhakikisha walimu wengi zaidi wanapata nafasi ya kuongeza maarifa na kuboresha ujuzi wao wa kitaaluma bila kuathiriwa na gharama za intaneti.

Farah ameongeza kuwa sekta binafsi ina nafasi muhimu katika kuharakisha maendeleo ya elimu kupitia uwekezaji katika teknolojia, miundombinu ya mawasiliano, vifaa vya TEHAMA na utaalamu wa kidijitali.

Amesisitiza kuwa ushirikiano wa wadau mbalimbali ni muhimu katika kujenga mfumo wa elimu unaokidhi mahitaji ya karne ya 21 na kuwawezesha walimu kuendana na mabadiliko ya teknolojia pamoja na mahitaji ya wanafunzi.

0 Hifadhi

Habari zinazohusiana

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

Top Stories · 20 Okt

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

Top Stories · 16 Okt

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

Top Stories · 16 Okt

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

Top Stories · 16 Okt

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Top Stories · 16 Okt

© 2026 Salamba TVMasharti ya matumiziSera ya faraghaSera ya marejeshoBeti kwa kuwajibika. Watu wazima 18+ pekee.

Shiriki kwa

Habari zinazohusiana

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

Top Stories · 20 Okt

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

Top Stories · 16 Okt

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

Top Stories · 16 Okt

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

Top Stories · 16 Okt

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Top Stories · 16 Okt

Zaidi kutoka

Top Stories →