Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema hatomuunga mkono Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, katika uchaguzi ujao wa Israel unaotarajiwa kufanyika Oktoba 27.
Akizungumza na jarida la TIME siku ya Alhamisi, Trump aliulizwa iwapo Netanyahu anapaswa kupewa muhula mwingine madarakani, ambapo alisema hataki kuhusika tena katika siasa za Israel, akisisitiza kuwa kipaumbele chake ni masuala ya ulinzi wa Israel.
Alipoulizwa moja kwa moja iwapo anamuunga mkono Netanyahu, Trump alijibu: “Hapana. Kipaumbele changu kikuu ni kutaka kuwasaidia kuilinda Israel.”
Kuhusu uwezekano wa Marekani kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na mgombea wa upinzani, Gadi Eisenkot, Trump alisema hajawahi kusikia mambo mabaya kumhusu, lakini akaonya kwamba Netanyahu hapaswi kupuuzwa.






