SalambaTV
NyumbaniHabariJamvikaRatibaRedio
  • Top Stories
  • Breaking News
  • Transfers
  • NBC Premier League
  • Match Highlights
  • Fixtures & Results
  • Standings & Tables
  • Tactical Analysis
NyumbaniHabariJamvikaRatibaRedio
SalambaTV
Ingia
Rudi nyumbani
Ingia

UHAMIAJI MARA WAENDELEA NA KAMPENI YA “MJUE JIRANI YAKO”

Salamba TV· Top Stories· 2 Oktoba 2026· 1 dakika za kusoma· 23 wasomaji
UHAMIAJI MARA WAENDELEA NA KAMPENI YA “MJUE JIRANI YAKO”

Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Mara imeendelea kutekeleza kampeni ya “Mjue Jirani Yako” kwa kutoa elimu kuhusu masuala ya uhamiaji kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi John Bosco, iliyopo Kata ya Mukendo, Musoma Mjini.

Zoezi hilo lililofanyika leo, Oktoba 2, 2026, lililenga kuwajengea wanafunzi uelewa kuhusu masuala ya uhamiaji, huduma zinazotolewa na Idara ya Uhamiaji pamoja na umuhimu wa kuwa na uelewa kuhusu watu wanaoishi katika maeneo yao.

Elimu hiyo ilitolewa na maafisa wa Uhamiaji wakiongozwa na Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji, Habiba Ally, akishirikiana na Konstebo Nassor Mohammed Khamis na Konstebo Sophia Ramadhan.

Akizungumza na wanafunzi hao, Habiba Ally alitoa elimu kuhusu uraia wa Tanzania na aina za uraia, huku akiwataka wanafunzi kufahamu wajibu wao kama raia.

Kwa upande wake, Konstebo Nassor Mohammed Khamis alieleza majukumu ya Idara ya Uhamiaji pamoja na masuala yanayohusu uhamiaji usiofuata taratibu za kisheria, ikiwemo sababu zinazoweza kuchangia uwepo wa wahamiaji wasio na hadhi halali nchini na madhara yake.

Naye Konstebo Sophia Ramadhan alitoa elimu kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na Idara ya Uhamiaji pamoja na taratibu zinazohusika katika kupata huduma hizo.

Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi John Bosco, Emmanuel Laurent Bilula, ameishukuru Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Mara kwa kutoa elimu hiyo, akisema imewajengea wanafunzi uelewa na kuwawezesha kuwa mabalozi wazuri katika kulinda Taifa na kushirikiana na mamlaka pale wanapohitaji kutoa taarifa.

0 Hifadhi

Habari zinazohusiana

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

Top Stories · 20 Okt

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

Top Stories · 16 Okt

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

Top Stories · 16 Okt

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

Top Stories · 16 Okt

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Top Stories · 16 Okt

© 2026 Salamba TVMasharti ya matumiziSera ya faraghaSera ya marejeshoBeti kwa kuwajibika. Watu wazima 18+ pekee.

Shiriki kwa

Habari zinazohusiana

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

Top Stories · 20 Okt

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

Top Stories · 16 Okt

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

Top Stories · 16 Okt

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

Top Stories · 16 Okt

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Top Stories · 16 Okt

Zaidi kutoka

Top Stories →