SalambaTV
NyumbaniHabariJamvikaRatibaRedio
  • Top Stories
  • Breaking News
  • Transfers
  • NBC Premier League
  • Match Highlights
  • Fixtures & Results
  • Standings & Tables
  • Tactical Analysis
NyumbaniHabariJamvikaRatibaRedio
SalambaTV
Ingia
Rudi nyumbani
Ingia

WAANDISHI WATAKIWA KUELIMISHA UMMA KUHUSU SERA YA TAIFA YA USIMAMIZI WA MNYORORO WA UGAVI

Salamba TV· Top Stories· 1 Oktoba 2026· 2 dakika za kusoma· 33 wasomaji
WAANDISHI WATAKIWA KUELIMISHA UMMA KUHUSU SERA YA TAIFA YA USIMAMIZI WA MNYORORO WA UGAVI

Serikali imewataka wanahabari kutumia kalamu zao na weledi wao kuongeza uelewa wa umma kuhusu Sera ya Taifa ya Usimamizi wa Mnyororo wa Ugavi, 2025, kwa kuzingatia takwimu sahihi, kueleza fursa zinazotokana na sera hiyo na namna inavyolenga kuimarisha matumizi bora ya rasilimali za umma.

MOROGORO: Serikali imewataka wanahabari kutumia kalamu zao na weledi wao kuongeza uelewa wa umma kuhusu Sera ya Taifa ya Usimamizi wa Mnyororo wa Ugavi, 2025, kwa kuzingatia takwimu sahihi, kueleza fursa zinazotokana na sera hiyo na namna inavyolenga kuimarisha matumizi bora ya rasilimali za umma.

Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Fedha, Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari na Wamiliki wa Mitandao ya Kijamii ya Habari, yaliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Timeless, mjini Morogoro.

Mhe. Munde amesema vyombo vya habari vina nafasi muhimu katika kujenga uelewa wa wananchi kuhusu sera hiyo na namna inavyohusiana na matumizi ya rasilimali za umma.

Amesema usimamizi wa mnyororo wa ugavi unahusisha hatua mbalimbali, ikiwemo utambuzi na upangaji wa mahitaji, ununuzi, ugomboaji, upokeaji, utunzaji na uhifadhi, matumizi, usambazaji pamoja na uondoshaji wa bidhaa, vifaa na mali.

“Usimamizi wa mnyororo wa ugavi una athari ya moja kwa moja katika namna rasilimali za umma zinavyotumika na namna huduma zinavyowafikia wananchi. Hivyo, Sera hii ni nyenzo muhimu katika kuimarisha ufanisi, uwajibikaji, uwazi na matumizi yenye tija ya fedha za umma katika shughuli za mnyororo wa ugavi katika Sekta ya Umma,” alisema Mhe. Munde.

Aidha, alisema utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Usimamizi wa Mnyororo wa Ugavi, 2025, unatoa fursa ya kuimarisha ushiriki wa wazalishaji, kampuni na watoa huduma wa ndani katika shughuli za mnyororo wa ugavi.

Kwa mujibu wa Mhe. Munde, hatua hizo pia zinalenga kuongeza matumizi ya bidhaa na huduma zinazozalishwa nchini, kuendeleza wataalamu wa ndani na kutumia teknolojia katika shughuli mbalimbali za mnyororo wa ugavi.

“Wahariri na waandishi wa habari ni kiungo muhimu kati ya Serikali, wadau na wananchi katika kufikisha taarifa hizi za kisera na kitaalamu kwa lugha rahisi na inayoeleweka. Ndiyo maana mpo hapa leo kupata uelewa zaidi kuhusu Sera hii,” alisema Mhe. Munde.

Aliongeza kuwa uelewa mpana wa wananchi kuhusu sera hiyo ni muhimu katika kuhakikisha jamii inafahamu namna mnyororo wa ugavi unavyohusiana na matumizi ya rasilimali za umma, utoaji wa huduma na maendeleo ya uchumi.

Mafunzo hayo ya siku mbili yanalenga kuwajengea uwezo Wahariri wa Vyombo vya Habari na Wamiliki wa Mitandao ya Kijamii ya Habari kuhusu Sera ya Taifa ya Usimamizi wa Mnyororo wa Ugavi, 2025, ili waweze kuifikisha kwa umma kwa usahihi, weledi na lugha inayoeleweka.

0 Hifadhi

Habari zinazohusiana

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

Top Stories · 20 Okt

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

Top Stories · 16 Okt

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

Top Stories · 16 Okt

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

Top Stories · 16 Okt

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Top Stories · 16 Okt

© 2026 Salamba TVMasharti ya matumiziSera ya faraghaSera ya marejeshoBeti kwa kuwajibika. Watu wazima 18+ pekee.

Shiriki kwa

Habari zinazohusiana

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

Top Stories · 20 Okt

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

Top Stories · 16 Okt

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

Top Stories · 16 Okt

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

Top Stories · 16 Okt

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Top Stories · 16 Okt

Zaidi kutoka

Top Stories →