SalambaTV
NyumbaniHabariJamvikaRatibaRedio
  • Top Stories
  • Breaking News
  • Transfers
  • NBC Premier League
  • Match Highlights
  • Fixtures & Results
  • Standings & Tables
  • Tactical Analysis
NyumbaniHabariJamvikaRatibaRedio
SalambaTV
Ingia
Rudi nyumbani
Ingia

WABUNGE EALA WAIpongeza SERIKALI KWA UJENZI WA UWANJA WA KISASA ARUSHA

Salamba TV· Top Stories· 12 Oktoba 2026· 3 dakika za kusoma· 34 wasomaji
WABUNGE EALA WAIpongeza SERIKALI KWA UJENZI WA UWANJA WA KISASA ARUSHA

Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) wameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji katika ujenzi wa uwanja wa kisasa jijini Arusha, ambao ni sehemu ya maandalizi ya Tanzania kuwa mwenyeji mwenza wa mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027.

Pongezi hizo zimetolewa wakati wabunge hao walipotembelea eneo la ujenzi wa uwanja huo na kujionea maendeleo ya mradi, huku wakieleza kuwa uwekezaji huo una nafasi kubwa katika kukuza michezo, utalii na uchumi wa Tanzania pamoja na nchi nyingine za Afrika Mashariki.

Akizungumza kwa niaba ya wabunge wenzake, Mbunge wa EALA, Cosato Chumi, amesema ujenzi wa uwanja huo ni hatua muhimu inayoonesha uwezo wa Tanzania kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati kupitia dhamira na uwekezaji wa rasilimali.

“Kwa kweli ni jambo kubwa, si jambo dogo. Huu ni uthibitisho kwamba Watanzania tukiamua tunaweza,” amesema Chumi.

Ameeleza kuwa maandalizi ya AFCON 2027 yanatoa fursa kwa Tanzania kuimarisha miundombinu ya michezo na kuweka msingi wa kuendelea kuwa mwenyeji wa mashindano makubwa ya kimataifa hata baada ya michuano hiyo kukamilika.

Chumi amesisitiza kuwa uwanja huo haupaswi kutumika kwa ajili ya AFCON pekee, bali unapaswa kuwa kituo cha kudumu cha kuandaa mechi za kimataifa, mashindano ya klabu na matukio mengine makubwa ya michezo.

Amesema ni muhimu kwa Serikali na wadau wa michezo kuanza mapema kuweka mikakati ya matumizi ya uwanja huo, ikiwemo kuandaa mashindano yatakayoshirikisha klabu kutoka Afrika Mashariki na Kati pamoja na timu kubwa kutoka sehemu mbalimbali za bara la Afrika.

Miongoni mwa klabu alizotaja kuwa zinaweza kualikwa kushiriki mechi za kirafiki na mashindano hayo ni Gor Mahia na AFC Leopards za Kenya, Mamelodi Sundowns na Kaizer Chiefs za Afrika Kusini, pamoja na Vipers na URA za Uganda.

Kwa mujibu wa Chumi, mashindano ya aina hiyo yatazipa klabu za Tanzania nafasi ya kupima uwezo wao dhidi ya timu zenye uzoefu wa kimataifa, hatua itakayosaidia kuongeza ushindani, kuboresha viwango vya wachezaji na kuinua ubora wa soka nchini.

Aidha, amesema uwanja huo una uwezo wa kuchochea utalii wa michezo mkoani Arusha kwa kuvutia wageni, mashabiki na wadau mbalimbali wa soka, ambao watatumia huduma za malazi, usafiri, migahawa na biashara nyingine.

Ameongeza kuwa ongezeko la wageni litafungua fursa za kiuchumi kwa wafanyabiashara na watoa huduma mbalimbali, huku vijana wakipata nafasi za ajira katika sekta zinazohusiana na michezo na utalii.

Kutokana na fursa hizo, Chumi amezitaka Serikali, wabunge, vyama vya michezo na sekta binafsi kushirikiana kuweka mikakati madhubuti ya kuhakikisha uwanja huo unatumika kwa tija na kuendelea kuleta manufaa kwa taifa kwa muda mrefu.

Amesema mipango ya kuandaa mashindano mengine ya kimataifa inapaswa kuanza kabla ya AFCON 2027 kumalizika ili kuepusha uwezekano wa miundombinu hiyo kutotumika kikamilifu baada ya mashindano.

Amebainisha kuwa uwekezaji katika miundombinu ya michezo ni fursa muhimu ya kukuza vipaji vya vijana na kuiweka Tanzania katika nafasi nzuri ya kushiriki na kuandaa mashindano makubwa ya kimataifa.

Ujenzi wa uwanja huo ni sehemu ya maandalizi ya Tanzania, Kenya na Uganda kuwa wenyeji wenza wa AFCON 2027, mashindano yanayotarajiwa kuongeza ushirikiano wa kikanda na kuitangaza Afrika Mashariki katika ramani ya soka la Afrika.

Matumizi endelevu ya uwanja huo yanatarajiwa kuwa muhimu katika kukuza michezo, kuimarisha utalii na kuchochea shughuli za kiuchumi, huku ziara ya wabunge wa EALA ikionesha umuhimu wa ushirikiano wa kikanda katika kutumia uwekezaji wa miundombinu kuleta maendeleo ya muda mrefu.

0 Hifadhi

Habari zinazohusiana

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

Top Stories · 20 Okt

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

Top Stories · 16 Okt

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

Top Stories · 16 Okt

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

Top Stories · 16 Okt

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Top Stories · 16 Okt

© 2026 Salamba TVMasharti ya matumiziSera ya faraghaSera ya marejeshoBeti kwa kuwajibika. Watu wazima 18+ pekee.

Shiriki kwa

Habari zinazohusiana

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

Top Stories · 20 Okt

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

Top Stories · 16 Okt

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

Top Stories · 16 Okt

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

Top Stories · 16 Okt

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Top Stories · 16 Okt

Zaidi kutoka

Top Stories →