SalambaTV
NyumbaniHabariJamvikaRatibaRedio
  • Top Stories
  • Breaking News
  • Transfers
  • NBC Premier League
  • Match Highlights
  • Fixtures & Results
  • Standings & Tables
  • Tactical Analysis
NyumbaniHabariJamvikaRatibaRedio
SalambaTV
Ingia
Rudi nyumbani
Ingia

Walimu zaidi ya 100 Rukwa wanufaika na mafunzo ya kidijitali kupitia DigiTruck ya Huawei

Salamba TV· Top Stories· 15 Oktoba 2026· 1 dakika za kusoma· 54 wasomaji
Walimu zaidi ya 100 Rukwa wanufaika na mafunzo ya kidijitali kupitia DigiTruck ya Huawei

Rukwa. Zaidi ya walimu 100 mkoani Rukwa wamenufaika na mafunzo ya ujuzi wa kidijitali kupitia mradi wa DigiTruck wa Kampuni ya Huawei Tanzania, yenye lengo la kuboresha ufundishaji.

Akihitimisha mafunzo hayo Oktoba 12, 2026, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Clement Sangu, alisema mradi huo unasaidia kupunguza pengo la ujuzi wa kidijitali na kuimarisha ubora wa elimu.

Mhe. Sangu alisema tangu uanze nchini mwaka 2024, mradi huo umefika katika mikoa 17. Mkoani Rukwa, mafunzo yametolewa kwa wiki tano katika shule za sekondari za Rukwa, Katuula, Uchile na Mpui, huku yakiendelea katika Shule ya Sekondari Mzindakaya.

Aliwataka walimu kutumia maarifa hayo kuandaa masomo yenye ubunifu na kutumia teknolojia kurahisisha ujifunzaji, akibainisha kuwa hatua hiyo inaunga mkono Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Waziri huyo aliipongeza Huawei kwa uwekezaji wa kijamii, huku akiwataka walimu walionufaika kushirikisha wenzao maarifa waliyoyapata.

Kwa upande wake, Meneja wa Mahusiano wa Huawei Tanzania, Boniface Leonard Ntimba, aliishukuru Serikali kwa ushirikiano na kuahidi kuwa kampuni hiyo itaendelea kushirikiana nayo kuendeleza mradi huo nchini.

Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari Rukwa Girls, Jane Kanyama, aliishukuru Serikali na Huawei kwa mradi huo, akisema una manufaa kwa shule, na kuomba urejee tena ili walimu wengi zaidi wanufaike.

DigiTruck ni darasa linalotembea lenye kompyuta 21, ubao janja, intaneti na nishati ya jua. Linalenga kufikisha mafunzo ya teknolojia kwa wananchi katika maeneo mbalimbali, ikiwemo ya vijijini.

0 Hifadhi

Habari zinazohusiana

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

Top Stories · 20 Okt

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

Top Stories · 16 Okt

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

Top Stories · 16 Okt

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

Top Stories · 16 Okt

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Top Stories · 16 Okt

© 2026 Salamba TVMasharti ya matumiziSera ya faraghaSera ya marejeshoBeti kwa kuwajibika. Watu wazima 18+ pekee.

Shiriki kwa

Habari zinazohusiana

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

Top Stories · 20 Okt

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

Top Stories · 16 Okt

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

Top Stories · 16 Okt

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

Top Stories · 16 Okt

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Top Stories · 16 Okt

Zaidi kutoka

Top Stories →