SalambaTV
NyumbaniHabariJamvikaRatibaRedio
  • Top Stories
  • Breaking News
  • Transfers
  • NBC Premier League
  • Match Highlights
  • Fixtures & Results
  • Standings & Tables
  • Tactical Analysis
NyumbaniHabariJamvikaRatibaRedio
SalambaTV
Ingia
Rudi nyumbani
Ingia

WRRB Yatoa Wito wa Kuzingatia Viwango vya Unyevu wa Korosho Msimu wa 2026/27

Salamba TV· Top Stories· 12 Oktoba 2026· 1 dakika za kusoma· 31 wasomaji
WRRB Yatoa Wito wa Kuzingatia Viwango vya Unyevu wa Korosho Msimu wa 2026/27

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB), Asangye Bangu, amewataka wakulima na waendesha maghala ya korosho kuhakikisha zao hilo linakaushwa na kuhifadhiwa kwa kuzingatia viwango vinavyotakiwa ili kudumisha ubora na thamani yake katika msimu wa mauzo wa 2026/27.

Bangu ametoa agizo hilo Oktoba 11, 2026, katika ghala la BUCO lililopo Masasi, mkoani Mtwara, linaloendeshwa na Kampuni ya Pugna, alipokuwa akihitimisha ziara maalum ya kukagua maghala katika mikoa ya Lindi na Mtwara.

Amesema ziara hiyo imelenga kutathmini utayari wa maghala kupokea na kuhifadhi korosho, pamoja na kuhakikisha yanachukua tahadhari zinazofaa kukabiliana na changamoto zinazoweza kusababishwa na mvua nyingi.

Kwa mujibu wa Bangu, ukaguzi huo umejumuisha hali ya paa na sakafu za maghala, mifumo ya kupitisha maji, mazingira ya uhifadhi, taratibu za kupokea korosho na uhakiki wa ubora pamoja na kiwango cha unyevu kinachokubalika.

Amesisitiza kuwa hatua hizo ni muhimu katika kuhakikisha korosho za wakulima zinahifadhiwa katika mazingira salama na kulindwa dhidi ya uharibifu unaoweza kuathiri ubora na bei ya zao hilo sokoni.

Aidha, amewataka wakulima kuhakikisha korosho zinakaushwa vizuri kabla ya kuzipeleka maghalani, huku waendesha maghala wakitakiwa kuzingatia masharti ya ubora wakati wa kupokea na kuhifadhi mazao hayo.

Amezitaka pia Jumuiya za Ushirika wa Wakulima (AMCOS) kuepuka kupokea korosho ambazo hazijakauka ipasavyo na kuendelea kutoa elimu kwa wakulima kuhusu mbinu sahihi za ukaushaji.

“Niwatake waendesha ghala kufanya ukaguzi wa mara kwa mara na kurekebisha mapungufu yanayoweza kuhatarisha usalama wa korosho, hususan kipindi cha mvua nyingi,” amesema Bangu.

Ameongeza kuwa WRRB itaendelea kuimarisha ukaguzi wa maghala na kushirikiana na wadau wa sekta ya korosho ili kulinda mazao ya wakulima na kuendeleza uaminifu katika Mfumo wa Stakabadhi za Ghala.

0 Hifadhi

Habari zinazohusiana

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

Top Stories · 20 Okt

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

Top Stories · 16 Okt

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

Top Stories · 16 Okt

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

Top Stories · 16 Okt

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Top Stories · 16 Okt

© 2026 Salamba TVMasharti ya matumiziSera ya faraghaSera ya marejeshoBeti kwa kuwajibika. Watu wazima 18+ pekee.

Shiriki kwa

Habari zinazohusiana

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

Top Stories · 20 Okt

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

Top Stories · 16 Okt

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

Top Stories · 16 Okt

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

Top Stories · 16 Okt

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Top Stories · 16 Okt

Zaidi kutoka

Top Stories →