SalambaTV
NyumbaniHabariJamvikaRatibaRedio
  • Top Stories
  • Breaking News
  • Transfers
  • NBC Premier League
  • Match Highlights
  • Fixtures & Results
  • Standings & Tables
  • Tactical Analysis
NyumbaniHabariJamvikaRatibaRedio
SalambaTV
Ingia
Rudi nyumbani
Ingia

ZUNGU: TANZANIA TAYARI KUSHIRIKIANA NA NCHI NYINGINE KUBORESHA AFYA YA MAMA NA MTOTO

Salamba TV· Top Stories· 12 Oktoba 2026· 2 dakika za kusoma· 44 wasomaji
ZUNGU: TANZANIA TAYARI KUSHIRIKIANA NA NCHI NYINGINE KUBORESHA AFYA YA MAMA NA MTOTO

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Azzan Zungu, amesema Tanzania iko tayari kushirikiana na nchi nyingine kwa kutoa uzoefu wake katika kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto mchanga, afya ya uzazi, lishe na ustawi wa vijana.

Zungu ameyasema hayo Oktoba 8, 2026, alipofungua mdahalo kuhusu afya ya mama na mtoto ulioandaliwa na Serikali ya Tanzania kwa wajumbe wanaoshiriki Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC).

Akizungumza katika mdahalo huo, Spika Zungu amesema afya na ustawi wa wanawake, watoto na vijana ni nguzo muhimu katika kufanikisha maendeleo ya taifa, akisisitiza umuhimu wa kuunganisha juhudi za kisiasa na ushirikiano wa kimataifa ili kuleta matokeo yanayodumu.

Amesema kila kifo kinachoweza kuzuilika, hitaji la kiafya lisilopatiwa ufumbuzi na kikwazo kinachomzuia mwananchi kupata huduma vinahitaji hatua madhubuti na dhamira endelevu kutoka kwa viongozi.

Zungu ameeleza kuwa Serikali ya Tanzania imeweka mkazo katika kupunguza vifo vya wajawazito na watoto, pamoja na kuhakikisha watoto wanapata huduma muhimu za chanjo.

Ameongeza kuwa juhudi hizo zinapaswa kuendelezwa ndani ya Tanzania na kusambazwa katika nchi nyingine za Afrika kupitia ushirikiano wa kikanda na mipango inayolenga kuimarisha afya ya mama na mtoto.

Akizungumzia nafasi ya mabunge katika kufanikisha malengo hayo, Zungu amesema wabunge wana wajibu wa kutunga sheria zinazolinda afya ya wananchi, kuhakikisha bajeti zinazotengwa zinatosheleza mahitaji na kusimamia matumizi ya rasilimali ili huduma ziwafikie walengwa.

Amesisitiza kuwa uwekezaji katika huduma za afya unapaswa kuzingatia usawa wa upatikanaji wa huduma za mama na mtoto mchanga, afya ya uzazi, lishe na ustawi wa vijana.

Aidha, amesema ushirikiano kupitia mitandao ya mabunge unaweza kuwawezesha viongozi kubadilishana uzoefu, kuimarisha uwajibikaji na kuweka mikakati ya pamoja ya kuboresha mifumo ya afya katika nchi zao.

Kwa upande wake, Mshauri wa Rais anayeshughulikia masuala ya afya, ustawi wa jamii, wanawake na watoto, Ummy Mwalimu, aliyemwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan, amesema bara la Afrika limepiga hatua katika kupunguza vifo vya kina mama, ingawa kiwango kilichofikiwa bado hakijakidhi mahitaji yaliyopo.

Mwalimu amesema takwimu zinaonesha kuwa vifo vya kina mama katika nchi wanachama wa Umoja wa Afrika vilipungua kwa asilimia 42 kati ya mwaka 2000 na 2023.

Hata hivyo, amebainisha kuwa Afrika bado inachangia takribani asilimia 70 ya vifo vya kina mama vinavyotokea duniani, hali inayoonesha umuhimu wa kuongeza uwekezaji na kuimarisha mikakati ya kuboresha huduma za afya ya uzazi.

Amesisitiza umuhimu wa kuendeleza juhudi za pamoja ili kupunguza vifo vinavyoweza kuzuilika na kuhakikisha wanawake, watoto na vijana wanapata huduma bora za afya kwa wakati.

0 Hifadhi

Habari zinazohusiana

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

Top Stories · 20 Okt

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

Top Stories · 16 Okt

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

Top Stories · 16 Okt

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

Top Stories · 16 Okt

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Top Stories · 16 Okt

© 2026 Salamba TVMasharti ya matumiziSera ya faraghaSera ya marejeshoBeti kwa kuwajibika. Watu wazima 18+ pekee.

Shiriki kwa

Habari zinazohusiana

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

ISRAEL MWENDA ARUDI KIKOSINI YANGA SC:

Top Stories · 20 Okt

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

STANBIC YAWAFIKIA WAFANYABIASHARA KARIAKOO KUHAMASISHA MALIPO YA YUAN KWA SHILINGI

Top Stories · 16 Okt

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

GWAJIMA AITAKA WIZARA KUONGEZA UWajibikaji NA MATOKEO KWA WANANCHI

Top Stories · 16 Okt

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

WATANZANIA WACHANGIA ASILIMIA 90 YA NGUVU KAZI MRADI WA UMEME MALANGALI

Top Stories · 16 Okt

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

SERIKALI YASEMA HAIWAKWAMISHI WAWEKEZAJI, YASISITIZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Top Stories · 16 Okt

Zaidi kutoka

Top Stories →